Peru yaripoti kisa cha Zika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtoto aliyeathiriwa na ugonjwa wa zika

Rais wa Peru Ollanta Humala, ametaka kuwepo kwa utulivu wa kiafya baada ya maafisa wa afya nchini humo kugundua kesi ya kwanza ya virusi vya Zika.

Amesema kuwa raia mmoja wa Venezuela aliyeambukizwa virusi hivyo nje ya mpaka wa Peru anatibiwa nyumbani kwake mjini Lima.

Zaidi ya mataifa 20 katika mabara ya Marekani yameathiriwa na virusi hivyo vinavyosambazwa na mbu.

Rais wa Marekani Barrack Obama na mwenzake wa Brazili Dilma Rousseff wamejadiliana jinsi ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Zika, ambavyo vimehusishwa na ongezeko la kasoro za uzazi.