Wapinzani Syria kuhudhuria mazungumzo Geneva

Geneva Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi ya wajumbe katika mazungumzo hayo ya Geneva

Kundi kuu la upinzani nchini Syria limesema litashiriki mazungumzo ya Amani ambayo yameanza mjini Geneva.

Kundi hilo linalojiita Kamati ya Mazungumzo ya Juu (HNC) ambalo linaungwa mkono na Saudi Arabia lilikuwa awali limesema lingeshiriki tu iwapo majeshi ya serikali ya Serikali yangesitisha mashambulio ya kutoka angani.

Aidha, lilitaka majeshi hayo ya serikali yaondoe uzio wa kijeshi katika miji inayodhibitiwa na makundi ya upinzani.

Mjumbe wa UN Staffan de Mistura tayari amekutana na wajumbe wa serikali ya Syria mjini Geneva.

Watu zaidi ya 250,000 wameuawa na 11 milioni kutoroka makwao kutoroka makwao tangu kuanza kwa vita hivyo vilivyodumu miaka mitano sasa.

Wanajeshi watiifu kwa Rais Bashar al-Assad na wanajeshi wa upinzani wanaendelea kukabiliana, huku wapiganaji wa kundi la Kiislamu linalojiita Islamic State (IS) pia wakipigana na kuteka maeneo.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Mamilioni ya watu wametoroka vita Syria

Mazungumzo ya sasa yanatarajiwa kuendelea kwa miezi sita, huku wajumbe wakikaa vyumba tofauti, maafisa wa UN wakifikisha mawasiliano kati ya makundi husika.

Mmoja wa wajumbe wakuu wa HNC amesema kundi hilo litatuma watu 30 au hata 35 kwa mazungumzo hayo ya Geneva, shirika la habari la AFP limeripoti.