Wahamiaji watoto elfu kumi wametoweka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji watoto elfu kumi wametoweka

Polisi wa Bara la Ulaya, Europol, wanasema wanakisia kuwa wakimbizi watoto kama elfu kumi (10,000) wametoweka tangu kuwasili Ulaya, na kuandikishwa na wakuu.

Afisa mmoja wa Europol, Brian Donald, ameliambia gazeti la Uingereza, la Observer, kwamba watoto kama elfu tano hivi 5,000 wametoweka Utaliano pekee yake.

Alisema ingawa Europol ina ushahidi kuwa magengi ya wahalifu yanawahadaa watoto hao walioko peke yao, lakini baadhi ya wahamiaji watoto pengine wamechukuliwa na jamaa zao.

Bwana Donald alisema Europol haijui watoto hao wako wapi, au wanafanya nini.