Mwanasiasa wa upinzani Uganda akamatwa

Image caption Jenerali mstaafu David Sejusa amekamatwa majuma 3 kabla ya uchaguzi

Mwanasiasa maarufu wa Uganda, Jenerali David Sejusa, amekamatwa, wiki tatu hivi kabla ya uchaguzi mkuu.

Wakili wake amesema askari jeshi waliizunguka nyumba yake leo alfajiri.

Inaarifiwa kuwa amewekwa katika kifungo cha nyumbani.

Jenerali Sejusa alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, anagombea uongozi tena katika uchaguzi wa tarehe 18 Februari.

Jenerali Sejusa, alikimbilia nchi za nje miaka mitatu iliyopita, baada ya kumshutumu rais Museveni, kuwa alikuwa akimuanda kimyakimya mwanawe kurithi uongozi.

Hii sio mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo kukamatwa, tangu kurudi Uganda.