Milipuko kadha yatokea Somalia

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Walioshuhudia wanasema kuwa walisikia karibu milipuko mitano.

Mtoto mmoja ameuawa na wengine sita kujeruhiwa kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu baada ya milipuko kulenga makao ya serikali yanayojumuisha ikulu ya rais.

Walioshuhudia wanasema kuwa walisikia karibu milipuko mitano.

Mtoto mmoja aliuawa wakati wa shambulizi hilo na wengine kadha kujeruhiwa.

Hakuna kundi lililodai kuendesha shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo la al-Shabab huendesha mashambulizi nchini Somalia kwa lengo la kuipindua serikali.

Muungano wa Afrika una karibu wanajeshi 22,000 wanaopigana na wanamgambo nchini Somalia.