Walioua dereva wa teksi Afrika Kusini wafungwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu kutoka mataifa mengine walivamia Afrika Kusini

Mahakama nchini Afrika Kusini imewahukumu wanaume wawili vifungo virefu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanamme mmoja raia wa Musumbuji wakati wa ghasia zilizokuwa zinawalenga watu wa mataifa mengine.

Mthinta Bhengu na Sifundi Mzimzela walihukumiwa miaka 17 na 10 mtawalia kwa kumuaa Emmanuel Sithole ambaye mauji yake yalinazwa na kamera mjini Johannesburg ilionyesha picha ya ghasia hizo za mwezi Aprili.

Jaji katika mahakama kuu mjini Johannesburg aliyataja mauaji kama ya kikatili.