50 wafa kwa kukosa hewa Sudan Kusini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali imekuwa ikikana vikali kuendesha ukatili wakati wa mzozo

Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini waliwaua watu 50 kwa kuwafungiandani ya behewa la mizingo nje ya jua kali, kwa mujibu wa waangalizi kwenye ripoti inayoangazia ukatili wa hivi punde wakati wa vita ambavyo vimedumua miaka miwili.

Kisa hicho kilitokea mwezi Oktoba katika jimbo la Unity.

Mabehewa hayo yaliyotangenezwa kwa chuma mara nyingi hutumuwa kama korokoroni nchini Sudan Kusini.

Serikali haijatamka lolote kuhusu madai hayo lakini siku za nyuma imekuwa ikikana vikali kuendesha ukatili wakati wa mzozo.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuhama makwao tangu mzozo huo uanze mwezi Desemba mwaka 2013.