Utaratibu wa kuchagua wagombea Marekani

Uchaguzi Haki miliki ya picha Getty
Image caption Majimbo yatawachagua wajumbe ambao mwishowe watachagua na kuidhinisha mgombea wa chama

Wanasiasa wanaotaka kuwania urais Marekani kupitia vyama mbalimbali wamekuwa wakikabiliana kwa miezi kadha sasa vyamani, lakini umefika wakati wa wananchi kuamua nani atapeperusha bendera.

Lakini je, ni utaratibu gani hufuatwa?

Mkutano wa kuwachagua wagombea uliofanyika Iowa ulikuwa wa kwanza katika msururu wa uchaguzi na mikutano katika majimbo yote ya Marekani.

Mchujo wa kuteua wagombea na umuhimu wake

Mshindi wa kila uchaguzi hupata wajumbe kadha, - wanachama wa chama ambao hukutana Julai kuidhinisha wagombea.

Mgombea anavyoshinda katika majimbo mengi, ndivyo anavyopata wajumbe wengi wa kumuunga mkono mkutano wa mwisho wa kuidhinisha wagombea.

Kwa kuwa Rais Barack Obama hawezi kuwania tena, vyama vyote viwili vinaanda uchaguzi kamilifu.

Mgombea wa Republican atahitaji wajumbe 1,237 ili kushinda, naye mgombea wa Democratic atahitajika kupata wajumbe 2,383.

Tofauti ni gani baina ya uchaguzi wa kuteua wagombea na mkutano wa kuteua wagombea

Kuna njia kadha tofauti za kuchagua wajumbe kupitia uchaguzi wa awali (primaries).

Uchaguzi ulio wazi hushirikisha wapiga kura wote waliojiandikisha katika jimbo husika, na wanaweza kupigia kura mgombea yeyote. Mpiga kura wa Republican anaweza kushiriki uchaguzi wa kuteua mgombea wa Democratic kwa mfano.

Katika uchaguzi usio wazi, ni wapiga kura wanachama wa chama pekee wanaoruhusiwa kushiriki.

Aidha, kuna uchaguzi mseto, ambapo wapiga kura wa chama pinzani hawaruhusiwi kushiriki lakini wapiga kura huru wanaruhusiwa kushiriki.

Mikutano ya kuteua wagombea (caucuses) ni mikutano ambayo huhusisha wapiga kura kuonyesha uungaji mkono wao kwa wagombea kwa kuinua mikono. Kawaida, ni wapiga kura waliosajiliwa pekee, ambao ni wafuasi wa chama husika cha siasa, hushiriki.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump anaongoza kwenye kura za maoni chama cha Republican

Hufanyika lini na wapi?

Uchaguzi wa awali wa kuteua wagombea huendelea hadi Juni, lakini uchaguzi wa mapema ndio husisimua sana kwani huashiria mwelekeo wa kinyang’anyiro.

Mbio hizi hufikia kilele kawaida tarehe 1 Machi au ‘Jumanne Kuu’ ambapo karibu majimbo 13 hufanya uchaguzi au mikutano ya kuteua wagombea siku moja.

Vyama vyote viwili huandaa uchaguzi wa awali au mikutano ya kuchagua wagombea siku moja, mara nyingi.

Februari:

Wagombea kujaribu kujijengea msingi na kusalia kwenye kinyang’anyiro.

1 Feb: Mikutano ya Iowa

9 Feb: Uchaguzi wa New Hampshire

20 Feb: Mikutano ya Nevada (Democratic), Uchaguzi wa South Carolina (Republican)

23 Feb: Mikutano ya Nevada (Republican)

27 Feb: Uchaguzi wa South Carolina (Democratic)

Machi:

Majimbo 13 hupiga kura Jumanne kuu ikiwa ni pamoja na majimbo sita Kusini. Ni nafasi nzuri kwa mgombea kujithibitishia ubabe, ingawa bado mambo huwa yanaweza kubadilika baadaye.

1 Machi – ‘Jumanne Kuu': Mikutano ya Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia Primaries; Alaska & Wyoming (Republican), Colorado Caucuses (Democratic)

5 Machi: Mikutano ya Kansas, Uchaguzi Louisiana, Mikutano Kentucky & Maine (Republican), Mikutano Nebraska (Democratic)

6 Machi: Mikutano ya Maine (Democratic)

8 Machi: Mikutano ya Hawaii & Idaho (Republican), Uchaguzi wa Idaho (Republican), Michigan & Mississippi

15 Machi: Uchaguzi wa Florida, Illinois, Missouri, North Carolina, Ohio

Kuna majimbo makubwa ambayo yatakuwa yakipigania mwezi Machi, hasa majimbo ambayo mshindi hupokea wajumbe wote. Pia kuna majimbo yasiyo na msimamo mkali ambako kuna uwezekano mkubwa kwa wagombea kuwashawishi wapiga kura kubadili msimamo.

22 Machi: Uchaguzi Arizona, Mikutano Utah, Mikutano Idaho (Democratic)

26 Machi: Mikutano ya Alaska, Hawaii, Washington Caucuses (Democratic)

Aprili-Mei

Haki miliki ya picha AP
Image caption Hillary Clinton anaongoza kwenye kura za maoni chama cha Democratic

Uchaguzi katika majimbo haya huenda ukawa muhimu zaidi kuliko kawaida kwa chama cha Republican kutokana na na kuwepo kwa wagombea waliofadhiliwa vyema mwaka huu, ambao wanaweza kusalia mbioni hadi Aprili.

1 Aprili: Mikutano North Dakota (Republican)

5 Aprili: Uchaguzi Wisconsin

9 Aprili: Mikutano ya Wyoming (Democratic)

19 Aprili: Uchaguzi wa New York

26 Aprili: Uchaguzi wa Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania, Rhode Island

3 Mei: Uchaguzi wa Indiana

10 Mei: Uchaguzi wa West Virginia, Uchaguzi wa Nebraska (Republican)

17 Mei: Uchaguzi Oregon, Uchaguzi Kentucky (Democratic)

24 Mei: Uchaguzi wa Washington (Republican)

Juni

7 Juni: Uchaguzi California, Montana, New Jersey, New Mexico, South Dakota; North Mikutano Dakota (Democratic)

14 Juni: Uchaguzi wa District of Columbia (Democratic)

18-21 Julai: Kongamano Kuu la Kitaifa la Wajumbe wa Chama cha Republican

25-28 Julai: Kongamano Kuu la Kitaifa la Wajumbe wa Chama cha Democratic