Maelfu ya wasafiri wakwama China

Image caption maelfu ya watu nje ya kituo cha reli

Theluji kubwa imechangia kukwama kwa mifumo ya usafiri wa umma kusini mwa China na kusababisha maelfu ya watu kukwama nje ya kituo cha reli.

Umati huo nje ya kituo cha Guangzhou uliongezeka hadi watu 100.000 ilipotimia Jumataua usiku. Eneo la kati kati mwa China limeshuhudia kipindi cha baridi kali baada ya miaka mingi.

Theluji hiyo isiyo ya kawaida imetokea wakati wa sherehe za mwaka mpya nchini China ambapo mamilioni ya wafanyikazi wahamiaji husafiri nyumbani kujiunga na familia zao.

Treli nyingi kutoka kaskazini na kati kati mwa China zilichelewa kufuatia kuwepo kwa theluji na kuwaacha abiria wengi wakiwa wamekwama maeneo ya kusini bila ya usafiri.