Jenerali Sejusa afikishwa mahakamani

Image caption Jenerali David Sejusa

Jenerali mwenye utata nchini Uganda David Sejusa amewasili katika mahakama moja ya kijeshi katika mji mkuu wa Kampala nchini Uganda.

Kulingana na mwandishi mmoja wa kampuni ya habari ya Nation Media ambaye amekuwa akituma ujumbe wa tweeter akiwa mahakamani haijajulikana ni mashtaka gani yanayomkabili.

Lakini siku ya jumatatu chombo cha habari cha Bloomberg kilimnukuu msemaji wa serikali Ofwono Opondo akisema kuwa Uganda inachunguza ripoti zinazomuhusisha jenerali mtoro David Sejusa na makundi yenye mipango ya kuzua ghasia.

Jenerali Sejusa aliwekwa katika kifungo cha nyumbani siku ya jumapili mjini Kampala.

Alikwenda mafichoni mnamo mwezi May 2013 baada ya kukosana na rais Yoweri Museveni ,lakini akarudi miezi 18 baadaye.

Alikuwa amemshtumu rais Museveni kwa kujaribu kutengeza ufalme wa kisiasa na kuongoza kwa kutumia mfumo wa kihuni.

Serikali imekana madai hayo.