Mos Def aomba kusalia Afrika Kusini

Image caption Mos Def na familia walikamatwa kwa kuishi nchini nchini Afrika Kusini kinyume na sheria.

Mwanamuziki raia wa Marekani wa mtindo aina ya rap Mos Def ambaye anakabiliwa na mashtaka nchini Africa Kusini chini ya kipengee cha uhamiaji atasalia nchi humo kwa muda mrefu.

Mwanamuziki huyo aliwasilisha ombi katika mahamaka ya Western Cape hii leo akitaka yeye pamoja na familia yake kuruhusiwa kubaki nchini humo.

Kesi yake inatarajiwa kusikilizwa mwezi Machi.

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake kamili ni Dante Smith, anajaribu kupata agizo ambalo litasababisha uwepo wake nchini Afrika kusini kuwa wa kudumu.

Aligonga vyombo vya habari mwezi uliopita wakati yeye na familia walikamatwa kwa kuishi nchini humo kinyume na sheria.