Wanariadha 8 wapigwa marufuku Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanne kati ya wanariadha walishinda dhahabu mwaka uliopita

Wanariadha wanane nchini Nigeria wamepigwa marufuku kutokana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Wanne kati ya wanariadha hao walishinda dhahabu katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika mwaka uliopita katika mji mkuu wa Congo Brazzaville.

Wanariadha hao walipigwa marufuku kwa miaka minne huku mmoja akipigwa marufuku ya miaka minane baada ya kupatikana na hatia ya kurudia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.