Somalia yachunguza mashambulizi ya Kenya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashambulia hayo ni kama ya kulipiza kisasi mashambulizi yaliyofanywa na al-Shabab

Serikali ya Somalia imeunda kamati kuchunguza madai ya vifo vya raia wengi vilivyosababishwa na mashambulizi ya angani ya kenya kusini mwa nchi hiyo.

Mashambulia hayo ni kama ya kulipiza kisasi mashambulizi yaliyofanywa na al-Shabab ambayo yalisababisha vifo vya idadi ya wanajeshi isiyojulikana katika mji wa el-Ade tarehe 15 mwezi Januari.

Kenya imekana madai ya wanamgambo kuwa raia wengi wameuawa lakini bado haijatoa idadi yake kamili.

Waziri wa ulinzi nchini Somalia Jenerali Abdilkadir Ali Dini, ambaye anaongoza uchunguzi huo alizungumza na BBC lakini hakutoa taarifa zaidi.

Kenya imechangia zaidi ya wanajeshi 4000 kwa wanajeshi 22,000 wa Muungano wa Afrika, ambao wako nchini Somalia kuisaidia serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kupigana na wanamgambo wa al-shabab.