Mahakama Misri yabatilisha hukumu ya vifo

wafuasi wa Muslim brotherhood Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafuasi wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood wakiwa gerezani

Mahakama nchini Misri imefuta hukumu ya kifo dhidi ya wafuasia 149 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood na kuamuru ianzishwe tena.

Watu hao walipatikana na hatia ya kufanya mashambulizi dhidi ya polisi mwaka 2013 kwenye kituo cha polisi cha Kerdasa, karibu na mji mkuu Cairo, ambapo polisi wapatao 11 waliuawa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohamed Badie akizungumza wakati wa kesi dhidi yake

Misri ilifanya msako mkali dhidi ya wanamgambo wa kiislam tangu jeshi lilipomg'oa madarakani rais Mohammed Morsi mnamo mwaka 2013.

Mamia ya wafuasi wake wamekua wakihukumiwa kifo katika kesi zinazohusisha watu wengi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Misri walivamia kambi ya waandamanaji wa Muslim Brotherhood wakati wa harakati za kudai mageuzi

Kesi hizo zilizua ukosoaji mkubwa kutoka kwa makundi ya haki za kibinadamu pamoja na Umoja wa Mataifa.

Morsi, ambae anatoka vugu vugu la Muslim Brotherhood, aliondolewa madarakani baada ya maandamano makubwa dhidi ya utawala wake

Tarehe 14 Agosti 2013,vikosi vya usalama vya Misri viliwavamia waandamanaji waliokua kwenye kambi zilizoandaliwa na wafuasi wa Muslim Brotherhood, na kusababisha vifo vya mamia ya watu.