Ushahidi dhidi ya Gbagbo waanza huko ICC

Haki miliki ya picha
Image caption Laurent Gbagbo ndiye Rais wa kwanza kufikishwa mbele ya ICC

Shahidi wa kwanza katika kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo ametoa ushahidi wake mbele ya mahakama ya kimataifa ya jinai-ICC.

Bwana Gbagbo amekanusha tuhuma za kutekeleza uhalifu wa kivita na dhuluma dhidi ya binadamu. Uhalifu huo umedaiwa kutekelezwa wakati wa machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu Ivory Coast mwaka wa 2010.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Gbagbo amekanusha kutekeleza uhalifu wa kivita

Shahidi huyo amesema kwamba alipigwa risasi kwa mguu na kisha akatandikwa na watu waliovalia sare za kijeshi wakati wa maandamano ya amani mji mkuu Abidjan.

Kuna taratibu zimewekwa kwa ajili ya usalama wa mashahidi japo shahidi wa leo alitaja jina lake bila kukusudia.