Georgia yatekeleza hukumu ya kifo

Brandon Astor John
Image caption Brandon Astor John alihukumiwa kifo miaka 36 iliyopia baada ya kupatikana na hatia ya kumuua meneja wa duka

Jimbo la Marekani la Georgia limetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mmoja wapo wa wafungwa mwenye wa miaka 72, akiwa ndie mfungwa alie kuwa na umri mkubwa zaidi katika jimbo hilo.

Brandon Astor Jones alihukumiwa kifo miaka 36 iliopita , baada ya kupatikana na hatia ya kumuua meneja wa duka wakati wa tukio la wizi.

Hukumu yake ilicheleweshwa kwa saa kadhaa baada ya wakili wake kuwasilisha rufaa dakika za kwisho kwenye mahakama kuu.

Georgia imewakwisha tekeleza hukumu ya kifo kwa watu 60 tangu mwaka 1976, na kuna makumi kadhaa ya watu walio wanaosubiri kuuawa.

Jones alipigwa sindano ya sumu mapema leo Jumatano katika gereza la Jackson, baada ya kukubali afanyiwe maombi ya mwisho.

Image caption Wanaomuunga mkono Brandon Astor John walipinga hukumu ya kifo dhidi yake

Yeye na mwanaume mwingine , Van Roosevelt Solomon, walipatikana na hatia ya kumuua meneja wa duka Roger Tackett wakati wa tukio la wizi mwaka 1979. Solomon aliuawa mwaka 1985.

Wanaomuunga mkono Jones wanadai alikana kumpiga risasi Bwana Tackett, na kwamba mahakama haikujali ushahidi kwamba alikua na matatizo ya kiakili na kuteswa kingiono alipokua mtoto .

Katika taarifa iliyotolewa kabla ya kuuawa, taarifa ya Kituo cha hukumu ya kifo ilisema , Jones alibakiza "wiki mbili atimize umri wa miaka 73 "na kwamba kesi yake '' inaibua maswali kuhusu uwiano na ubaguzi katika utoaji wa hukumu ya kifo".

Jaji wa Mahakama kuu alibadilisha uamuzi wa hukumu ya kifo dhidi ya John mwaka 1989, akisema jopo la mahakama walileta biblia kinyume cha taratibu katika chumba cha mahakama, suala ambalo hue4nda lilishawishi uamuzi wao.