Wahamiaji wa Afrika wasiotakiwa na Israel

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wahamiaji wa Israel

Kwa muda wa mwaka mmoja sasa Israel imekuwa ikiwapatia wahamiaji kutoka Afrika fedha ili kwenda kuishi vizuri katika taifa jengine.

Serikali ya Israel ina mkataba na matafa mawili ya Afrika ambayo yatawahifadhi wahamiaji hao wasiotakikana nchini humo.

Israel imekataa kuyataja mataifa hayo mawili ya Afrika, lakini BBC imezungumza na wahamiaji hao ambao wanasema walitumwa nchini Uganda na Rwanda.

Imeahidi kwamba wale watakaokubali mpango huo watapewa makaratasi wanapowasili ambayo yatawapa uraia katika taifa hilo.

Kama kiinua mgongo, wahamiaji hao hupewa dola 3,500 pesa taslimu ambazo hutolewa katika eneo la kusafiri katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv.

Lakini BBC imezungumza na watu wawili ambao wanasema walitupiliwa mbali baada ya ndege yao kuondoka.

Mmoja wao aliuzwa huku aliyesalia akiamua kupigania maisha yake bila ya vibali.