Chanjo za polio zateketezwa Kenya

muundo wa kirusi cha polio Haki miliki ya picha LFRYDEPT STRUCTURAL BIOLOGYOXFORD
Image caption Muundo ya virusi vya chanjo inayotibu maradhi ya polio

Taasisi ya Utafiti wa tiba ya Kenya (KEMRI) imeteketeza shehena za chanjo ya maradhi ya polio aina ya pili PolioVirus type 2 (WPV2) katika tukio la kihistoria.

Chanjo hiyo huundwa kwa kutumia virusi vya maradhi ya polio vilivyodhoofishwa ili kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya maradhi ya polio ya aina hiyo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Afrika sasa haina maradhi ya polio aina ya pili

Kwa mujibu wa taarifa yake kwa vyombo vya habari KEMRI imesema. "juhudi za kupambana na maradhi ya polio barani Africa zimefikia viwango muhimu, ambapo bara la Africa halina taifa linalokabiliwa na aina hiyo ya maradhi ya polio. Mwaka wa 2015 Nigeria ilitangazwa kuwa haina tena maradhi ya polio."

Tume ya dunia ya kutoa vyeti vya udhibitisho ilidhibitisha kuangamizwa kwa maradhi ya polio ya aina ya pili na kutangaza rasmi mwezi Septemba mwaka 2015 kuharibiwa kwa chanjo za maradhi hayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chanjo za polio zimeteketezwa kuangamiza maradhi ya polio aina ya pili

Chanjo hizo zimeteketezwa ili kuzuia kuibuka tena kwa maradhi hayo ya polio ya aina ya pili, kwa hofu kuwa huenda zikatumika kwa ugaidi wa kiafya, na ili kuangamiza kikamilifu hazina ya vimelea vya maradhi hayo.

Maabara ya polio ya shirika la KEMRI imetambuliwa kuwa na virusi vinavyotumiwa kutibu polio aina ya (WPV1) na (WPV3) ambavyo vina uwezo wakusababisha mlipuko wa maradhi ya polio endapo vitatolewa kwa umma kimakosa ama kwa kukusudia.