Wataka Neymar ashtakiwe na ufisadi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Neymar

Waendesha mashtaka nchini Brazil wamependekeza kwamba nyota wa timu ya Barcelona Neymar ashtakiwe na mashtaka matatu ya ufisadi kuhusu kesi ya kodi wakati wa uhamisho wake hadi Barcelona.

Inadaiwa kwamba kampuni zilibuniwa ili kutumika kwa niaba yake ili mchezaji huyo alipe kodi ya kiwango cha chini.

Maafisa nchini Brazil wanasema kuwa madai hayo dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona yanasimamia kipindi cha miaka saba kuanzia 2006.Madai hayo ni tofauti na yale ya kesi iliosikizwa siku ya Jumanne nchini Uhispania.

Neymar alihudhuria kesi yake ya madai ya ufisadi kuhusu uhamisho wake.Amekana kufanya makosa yoyote.

Waendesha mashtaka wa serikali ambao wanapendekeza kushtakiwa kwake wanadai kwamba kampuni zilibuniwa na fedha ambazo zingelipishwa kodi katika kiwango cha mtu binafsi zilitumwa katika kampuni hizo ili kupunguza ada hiyo.

Ni mapema mno.

Madai hayo ya viongozi wa mashtaka yatakwenda kwa jaji ambaye ataamua iwapo kuna kesi ya kujibu au la.kwa sasa Neymar sio mshtakiwa.