Matrilioni ya dola yaliyoporwa yafichuliwa Nigeria

Dollar Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtawala wa zamani wa Nigeria Sani Abacha aliiba dola zaidi ya milioni 2 mwaka 1998 pekee

Kwa miaka 12 iliyopita Nigeria imeweza kufichua zaidi ya dola trilioni 2 zilizokua zimeporwa kutoka hazina ya taifa , amesema waziri wa sheria wa nchi hiyo Abubakar Malami .

Magenge ya wahalifu na wakuu wa ofisi za umma waliiba pesa, aliongeza kusema.

Mwaka 1998 pekee, mtawala wa kijeshi Sani Abacha alipora zaidi ya dola milioni 2, Bwana Malami amenukuliwa na gazeti la Nigeria-Vanguard akielezea.

Rais Muhammadu Buhari ameapa “kurejesha mali ambazo wahalifu walizipora kwa kurejesha kila pesa ambayo ni mali ya umma nchini Nigeria ”, Aliongeza kusema waziri Malami .