Rand Paul hawanii tena urais Marekani

Paul Rand Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Paul Rand ametangaza kujiengua kwenye mchuano wa uchaguzi kwa tiketi ya Republican

Seneta wa chama cha Republican amejiondoa kwenye mchujo wa kuelekea uchaguzi wa urais nchini Marekani baada ya kukata tamaa alipokuwa watano katika kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi huo katika jimbo la Iowa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mara kwa mara Senetor Paul Rand alilumbana na mahasimu wake juu ya mawazo yao ya sera za nje

Mara kwa mara Paul alilumbana na mahasimu wake wa Republican kuhusiana na maoni yao juu ya sera ya kigeni na uungaji mkono wao wa mpango wa serikali wa uchunguzi wa kisiri . Amesitisha nia yake kama sehemu ya mpango wake wa kuwania kuchaguliwa tena katika kiti cha useneta .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Senetor Paul Rand anawania tena useneta

Anaonekana kama mtu anaewakilisha kambi ya wenye kupendelea mabadiliko ya wastani ya chama chake, wanaopendelea kuwepo kwa haki za watu binafsi na usiri wa mtu .

"kote nchini Marekani maelfu kwa maelfu ya watu wamekua wakivamia ujumbe wetu ambao si wa serikali, wa siri , mageuzi kuhusu mfumo wa sheria wa uhalifu na sera ya maana ya kigeni ," alisemahe. "ingawa, leo nitasitisha kampeni zangu Aza urais, nitapigania haki za mabadiliko.