Abiria ajipata pekee yake katika ndege ya China

Haki miliki ya picha Weibo Miffyscat
Image caption Abiria ajipata pekee yake katika ndege ya China

Mwanamke mmoja raia wa China aliyekuwa amesubiri ndege kwa kipindi kirefu alibahatika na kuwa abiria wa pekee katika ndege hiyo.

Bi Zhang alikuwa miongoni mwa zaidi ya abiria laki moja waliokwama katika uwanja wa ndege kufuatia kimbunga kikali kilichokumba maeneo mengini ya China katika kipindi cha siku mbili zilizopita.

Zhang alikuwa amenunua tikiti ya ya kuelekea nyumbani kwa katika mji wa Guangzhou ilikusheherekea na jamaa zake sikukuu ya mwaka mpya ya kichina.

Hata hivyo hali ya hewa ilipokuwa shwari abiria wengine walibadilisha ndege yao na kusafiri huku wakimwacha bi Zhang nyuma.

Haki miliki ya picha WEIBO
Image caption Bi Zhang alikuwa miongoni mwa zaidi ya abiria laki moja waliokwama katika uwanja wa ndege kufuatia kimbunga kikali kilichokumba maeneo mengini ya China

Mwishowe wakati wa ndege yake ilipowadia Zhang alijipata kasalia pekee yake.

Yaani dada huyo alikuwa ni yeye pekee na wahudumu wa ndege.

Hakukuwa na swala la kutafuta kiti wala kilio cha watoto wanaowasumbua wazazi wao , Zhang alikuwa na uhuru wa kuketi katika kitengo cha mabwenyenye yaani ''First Class'' ama akitaka akwende akaketi kule nyuma .

Haki miliki ya picha WEIBO
Image caption Mwishowe wakati wa ndege yake ilipowadia Zhang alijipata kasalia pekee yake.

Kokote alikotaka aliketi na hukohuko alihudumiwa kama bwenyenye anayemiliki ama aliyekodisha ndege kwa sababu ya safari binafsi !

Amini usiamini ilikuwa safari ya kipekee maishani mwake !

Na kwa sababu hakutaka isahaulike alirusha picha zikiandamana na maelezo katika mtandao wa kijamii wa Weibo.

''Ninahisi kama msanii nyota !!

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Zhang alilipa dola 181 pekee kwa safari hiyo.

Sio jambo la kawaida kulipa nauli ya kawaida kisha ukajipata ni wewe pekee yako'' aliandika bi Zhang.

Zhang alilipa dola 181 pekee kwa safari hiyo.

Maelfu ya wafuasi wake walimsifu sana na haswa wahudumu wa ndege na rubani waliohakikisha siku hiyo ya kipekee inamwendea sawa sawa abiria wao spesheli.