Obama awakemea wanaoshtumu Waislamu

Haki miliki ya picha AP
Image caption Obama katika kikao na Waislamu

Rais Barrack Obama ameshtumu kile alichokitaja kuwa matamshi machafu dhidi ya Uislamu, kufuatia tamko la hivi majuzi lililotolewa na mgombea wa urais kupitia tiketi ya Republican Donald Trump.

Katika ziara yake ya kwanza katika msikiti kama rais, Obama amesema kuwa matamshi machafu dhidi ya waislaumu hayakubaliki nchini Marekani.

Aliwapongeza Wamarekani Waislamu kama walio na heshima na uzalendo wa hali ya juu na taifa lao. Bw Trump ametoa wito kwa waislamu kutoruhusiwa kuingia nchini Marekani.

Obama alikuwa akizungumza katika msikiti wa jamii ya waislamu mjini Baltimore Maryland.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Barrack Obama

Ametembelea misikiti katika maeneo mengine ya dunia katika ziara rasmi katika kipindi chake cha miaka saba akiwa rais.

Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa ziara hiyo ni kutetea uhuru wa kidini na matamshi ya kutovumiliana dhidi ya jamii za walio wachache.

Obama amesema kuwa anajua kwamba Waislamu Wamarekani wanalengwa na kulaumiwa kwa vitendo vya wachache.

''Wamarekani wengi hawawajui Waislamu'', alisema. Wengi huwasikia Waislamu na Uislamu kutoka kwa vyombo vya habari baada ya tendo la ugaidi ama katika chombo cha habari kinachoouangazia Uislamu, TV ama hata katika filamu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais Obama akiwa katika ziara ya msikitini nchini Misri

Rais Obama amekuwa na uhusiano wa kutatiza na Waislamu. Mapema katika uongozi wake aliapa kuimarisha uhusiano na Waislamu katika mataifa ya kigeni baada ya vita vya Iraq.