Familia ya Savimbi yaishtaki ''Call of Duty''

Image caption Video ya mchezo wa Call of Duty

Familia ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi imewashtaki watengezeji wa filamu ya Call of Duty kuhusu vile ilivyomuangazia katika mchezo huo wa video.

Watoto 3 wa Savimbi wanamtuhumu Activision Blizzard kwa kumuonyesha kama mtu 'mshenzi'.

Wanataka kulipwa dola milioni 1.1 kama malipo ya kumuaharibia jina baba yao.Hatahivyo Activision anasema kuwa kanda hiyo ni ''nzuri''.

Savimbi ndio mwanzilishi wa Vuguvu la Unita,lililotekeleza vita vya muda mrefu na serikali ya Angola.

Angola ilibadilika na kuwa taifa la vita baridi ,Vuguvugu hilo likiungwa mkono na Marekani pamoja na serikali ya ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini huku chama tawala cha Angola kikiungwa mkono na muungano wa Sovieti pamoja na serikali ya Cuba.

Kiongozi huyo wa waasi baadaye aliuawa katika vita na majeshi ya serikali mwaka 2002.