Wanasayansi watangaza vita dhidi ya kunguni

Image caption Kunguni

Wanasayansi wameorodhesha vinasaba vya DNA vya kunguni ili kusaidia kumuangamiza mdudu huyo, ambaye amekuwa akijenga kinga dhidi ya dawa za wadudu.

Matokeo yanaonyesha mdudu huyo anavyoweza kuishi kwa kutengeneza viumbe vinavyokabiliana na sumu ya dawa hizo.

Mdudu huyo pia ameanza kumea ngozi nzito ambayo huwasaidia kujilinda dhidi ya shambulio la kemikali.

Hatahivyo kuna awamu ya maisha yake ambapo ni huenda ikawa rahisi kumuua.

Hii ni kulingana na makundi mawili ya wanasayansi walio na kambi zao kuu katika jengo la makumbusho la Marekani ,Chuo kikuu cha Cincinati pamoja na Taasisi ya Baylor mjini Texas.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wanasayansi

Huyo ni kunguni mdogo ambaye hajawahi kuonja tone la damu ya binaadamu.

Kunguni huishi kwa kunywa damu ,na ni hadi mdudu huyo anapoanza kula ndiposa baadhi ya vinasaba vyake vya DNA vinavyomlinda dhidi ya dawa hizo huanza kujiimarisha.