LeBlanc mtangazaji mwenza wa Top Gear

Image caption LeBlanc kuwa mtangazaji mwenza wa Top Gear

Aliyekuwa msanii nyota wa kipindi cha Friends, Matt LeBlanc ameteuliwa kuwa mtangazaji mwenza wa kipindi cha magari cha Top Gear.

LeBlanc abaye ni mzaliwa wa Marekani atakuwa mtangazaji mweza wa kipindi hicho ambaye siye raia wa Uingereza.

Kipindi hicho kitarejea hewani tena mapema mwezi Mei.

Tangazo hilo limemfurahisha mtangazaji mwenza Chris Evans ambaye amemsifu sana mMarekani huyo akisema kuwa

''Ni vyema kupatana na kushirikiana na mtu anyependa harufu ya Petroli na Le Blanc ni mmoja kati ya wale wanaofahamu na kutambua mlio wa gari''

Watayarishi wengine na mtangazaji wa tatu atatangazwa karibuni na shirika la BBC.

Le Blanc anasema kuwa '' Ni jambo la kujivunia sana kuwa mmoja wa watangazi wa kipindi hiki chenye ufuasi mkubwa sana kote duniani''

''Natumai nitakisaidia kuimarika hata zaidi.''

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kikosi hiki kipya cha watangazaji kinatarajiwa kuendeleza kipindi hicho baada ya kutimuliwa kwa Jeremy Clarkson kwa utovu wa nidhamu.

Le Blanc mwenye umri wa miaka 48 alipata sifa kwa mara ya kwanza akifahamika kama Joey Tribbiani katika kipindi cha runinga cha Friends.

LeBlanc aliwahi kushiriki katika maonyesho mawili ya kipindi cha Top Gear kama msanii nyota anayeendesha gari la kawaida tu.

Kaimu mkurugenzi wa usanii wa shirika la BBC Alan Tyler alisema kuwa nyota yake itang'aa zaidi kama mtangazaji mweza wa Top Gear.

''yeye tayari ni nyota na kumsajili kama mtangazaji wa Top Gear ni jambo la kujivunia''

Kikosi hiki kipya cha watangazaji kinatarajiwa kuendeleza kipindi hicho baada ya kutimuliwa kwa Jeremy Clarkson kwa utovu wa nidhamu.