Brazil yatangaza vita dhidi ya Zika

Mbu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Virusi vya Zika vinasambazwa na mbu aina ya Aedes

Rais wa Brazil Dilma Rousseff ametangaza vita dhidi ya mbu wanaosambaza virusi vya Zika katika ujumbe uliorekodiwa kwenye Televisheni.

Amesema siku ya uhamasishaji kuhusu vita hivyo itakua Jumamosi, ambapo maelfu ya wanajeshi na wafanyakazi wa umma watafanya kazi ya kuwaangamiza wadudu katika makazi ya watu na ofisi.

Bi Rousseff amesema wengi kati ya mbu wanazaliana ndani ama karibu na nyumba za watu.

Zika umekua ukihusishwa na watoto wanaozaliwa na ubongo ambao haujakomaa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Brazil Dilma Rousseff aahidi kwamba raslimali za taifa zitatumika kuwaangamiza mbu wanaosambaza Zika

Virusi vya ugonjwa huo vinasambaa kupitia wamarekani na shirika la afya duniani (WHO) limetangaza ugonjwa huo kuhusianakuwa janga.

Katika hotuba yake, Bi Rousseff amesema kwamba raslimali za kitaifa zinatolewa kwa ajili ya kukabiliana na mbu aina ya Aedes wanaosababisha ugonjwa huo, kwasababu ni vita ambavyo, "haviwezi kushindwa". "sote kwa pamoja tunapaswa kushiriki katika vita hivi ," alisema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Serikali itawasaidia watoto walioathirika na Zika pamoja na familia zao

"tunahitaji msaada na utashi kutoka kwa kila mtu. Shirikianeni, kuhamasisha familia zenu na jamii zenu .

"nitasisitiza, kwasababu sayansi haijaweza kutengeneza chanjo dhidi ya virusi vya Zika, njia pekee inayofaa ya kuzuia ugonjwa huu ni vita vikali dhidi ya mbu."

Rais huyo pia alisema kwamba anataka hasa kutuma "ujumbe wa kuwaliwaza " wakina mama na akina mama watarajiwa.

"tutafanya kila liwezekanalo , lililo chini ya uwezo wetu kuwalinda . Na tutafanya kila tuwezalo kuwapa usaidizi watoto walioathirika na Zika na familia zao ."