El Chapo:Mexico yamsaka nyota wa filamu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kate Del Castillo

Waendesha mashtaka nchini Mexico wametoa agizo la kumtafuta ili kumhoji nyota wa filamu Kate del Castillo kuhusu uhusiano wake na mlanguzi wa mihadarati Joaquin El Chapo Guzman.

Nyota huyo wa filamu nchini Mexico alipanga mkutano kati ya nyota wa Hollywood Sean Penn na Guzman,ambaye alikuwa ametoroka wakati huo.

Waendesha mashtaka wanasema kwamba huenda alipewa fedha na Guzman ili kuanzisha biashara yake ya Tequila mwaka uliopita.

Bi. Del Castillo ambaye pia ana uraia wa Marekani,alipigiwa simu ili ahojiwe mda mfupi baada ya kukamatwa kwa El Chapo.

Lakini alikataa kujiwasilisha katika ubalozi wa Mexico mjini Los Angeles,ambapo anaishi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption El Chapo Guzman

Agizo hilo jipya linaweza kufanyika katika himaya ya taifa la Mexico pekee.

Iwapo atarudi katika taifa lake alikotoka,atakamatwa na kuzuia ili kuhojiwa kama shahidi.

Wakili wake nchini Marekani,Harland Braun,amesema kwamba bi Del Castillo anajiandaa kuzungumza na mamlaka iwapo atapata taarifa kamili.''Hafichi lolote.Hakuna tatizo la kumtafuta.Kila mtu anajua ana mawakili,wazungumzaji wake na mawakala,''Braun aliliambia shirika la habari la AP.