Wazazi wa ''Jihad Jack'' wakamatwa

Image caption Jack Letts

Wazazi wa raia mmoja wa Uingereza ambaye aliripotiwa kusafiri hadi nchini Iraq ili kujiunga na Kundi la Islamic State wamebaini kwamba walikamatwa na maafisa wa polisi.

Jack Lets mwenye umri wa miaka 20 kutoka Oxford,ametajwa kuwa ''Jihadi Jack'' na magazeti kadhaa,ambayo yameripoti kwamba aliondoka nchini Uingereza ili kujiunga na kundi hilo wakati alipokuwa na miaka 18.

John na Sally Letts walikiambia chombo cha habari cha Channel 4 kwamba walikamatwa baada ya kumtumia fedha za chakula na miwani mipya.

Image caption John Letts babaake Jihad jack

Maafisa wa polisi wa Thames Valley wamethibitisha kuwa iliwakamata wazazi hao.

Msemaji amesema kuwa :Mwanamume mmoja wa miaka 55 na mwanamke wa miaka 53 kutoka Oxford walikamatwa kwa tuhuma za kutuma fedha nchini Syria ambazo zitatumika kwa maswala ya kigaidi,na waliotolewa hadi februari 17.