Ouattara: Hatutapeleka watu tena ICC

Ouattara Haki miliki ya picha
Image caption Ouattara alichaguliwa tena kuongoza Ivory Coast mwaka jana

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema raia wa nchi hiyo hawatapelekwa tena mahakama ya kitaifa ya uhalifu wa kivita (ICC) mjini The Hague, Uholanzi.

Kiongozi huyo amesema Ivory Coast sasa ina mfumo wa mahakama unaofanya kazi.

Bw Ouattara alikuwa akizungumza mjini Paris baada ya kukutana na Rais wa Ufaransa Francois Hollande.

Amesema kesi zitakuwa zikishughulikiwa na mahakama za kitaifa nchini Ivory Coast.

Haki miliki ya picha
Image caption Gbagbo anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC

Mpinzani wa muda mrefu wa bw Ouattara, Laurent Gbagbo, kwa sasa yumo ICC ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi wa 2010.

Bw Gbagbo amekanusha mashtaka hayo.

Mahakama ya ICC imetuhumiwa na baadhi ya watu Afrika kwamba inaonea bara hilo.