Al-Shabab wachukua mji wa Merca, Somalia

Haki miliki ya picha d
Image caption alshabaab

Gavana wa jimbo la Shebelle nchini Somalia amethibitisha kuwa wapiganaji wa al-Shabab wamechukua udhibiti wa mji wa Merca kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Umoja wa Afrika.

Vikosi hivyo viliondoka katika mji huo na wapiganaji wa al-Shabab wakaingia, na sasa wamechukua udhibiti bila ya kumwaga damu,kulingana na Ibrahim Said, shirika la habari la AFP limetangaza.

Vikosi vya Umoja wa Afrika viliudhibiti mji huo wa Bandari kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu.

Wachanganuzi wanasema kuwa upotezaji wa mji huo ni pigo kubwa kwa vikosi vya AU katika vita vyake vya karibu mwongo mmoja dhidi ya alshabaab.