Kwa Picha: Magari mapya ya polisi wa Uganda

Magari Polisi
Image caption Uchaguzi mkuu nchini Uganda utafanyika Februari 18

Serikali ya Uganda imenunua magari mapya ya kutumiwa na maafisa wa polisi, baadhi yakiwa ya kukabiliana na fujo, huku taifa hilo likijiandaa kwa uchaguzi mkuu.

Magari hayo ambayo ni takriban 30 yamewasili wiki hii katika bandari ya Mombasa.

Yanatarajiwa kusafirishwa hadi Uganda karibuni. Aprili 2014, jeshi la polisi nchini Uganda liliomba pesa zidi kutoka kwa Bunge kununua vifaa na magari ya kusaidia kukabiliana na machafuko katika mwaka wa kifedha wa 2015/2016, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya.

Uchaguzi mkuu nchini Uganda utafanyika Februari 18.

Rais Yoweri Museveni, ambaye ameongoza taifa hilo tangu 1986, anakabiliwa na upinzani kutoka kwa kiongozi wa FDC Kizzaa Besigye na aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi.

Majuzi, Kenya pia ilinunua magari mapya ya kutumiwa na maafisa wa polisi. Magari hayo yaliyozinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta yatatumiwa sana kulinda maeneo ambayo yamekuwa yakishambuliwa na magaidi.

Haki miliki ya picha PSCU