Virusi vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo

Haki miliki ya picha Edmar Melo JC Picture
Image caption Mtoto aliyeathirika ka virusi vya Zika

Virusi hai vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo ya wagonjwa,wanasayansi wa Brazil wamesema.

Matokeo hayo hayamaanishi kwamba ugonjwa huo unaweza kusambazwa kupitia maji maji hayo ya mwilini.Sababu kuu ya kuenea kwa virusi hivyo ni kupitia kuumwa na mbu,lakini wanasayansi wanachunguza njia nyengine.

Huku maambukizi ya Zika yakiwa sio makali,ugonjwa huo umehusishwa na maelfu ya watoto waliozaliwa na kasoro.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Harakati za kukabiliana na Zika

Virusi vya Zika pia vimepatikana katika majimaji mengine ya mwilini katika mripuko mwengine uliotokea eneo la Polynesia,lakini mamlaka ya Brazil inasema kuwa hii ni mara ya kwanza virusi hai vya Zika kupatikana.

Paula Gadelha,mkuu wa taasisi ya Fiocruz ambayo inashirikiana na wizara ya Afya amesema:''Virusi hivyo vya Zika vimepatikana katika Mate na mikojo''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanasaynsi wa Brazil

''Lakini hiyo hainamishi kwamba kuna uwezekano wa kuenea kwa virusi hivyo kupitia mate na mikojo.Hatari ya kuenezwa kwa virusi hivyo kupitia maji maji ya mwilini uliangaziwa nchini Marekani ambapo kituo cha udhibiti wa magonjwa kinaamini kisa kimoja kilisambazwa kupitia ngono''.

Hatahivyo kumekuwa na kesi mbili pekee za usambazaji wa virusi hivyo kupitia ngono.