AU yaitaka Burundi kukubali wanajeshi wake

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Chad Idris Deby ndio mwenyekiti wa AU

Muungano wa Afrika, AU, umetoa wito kwa viongozi wa mataifa matano kuishawishi Burundi kukubali kikosi maalum cha kudumisha amani kufuatia miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini humo.

Kamati hiyo maalumu ya AU, inamshirikisha Waziri Mkuu wa Ethiopia, pamoja na Marais wa Afrika Kusini, Mauritania, Gabon na Senegal.

Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Burundi

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amepinga mpango huo, akisema huo ni uvamizi.

Uamuzi wake wa mwaka uliopita kutaka kugombea awamu ya tatu ulianzisha mapigano hayo ambapo kufikia sasa mamia ya watu wameuawa.

Haki miliki ya picha
Image caption Viongozi wa Umoja wa Afrika

Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana juma lililopita walighairi juu ya swala la kuwatuma wanajeshi 5,000 wa kudumisha amani, na badala yake wakaamua kutumia njia za kidiplomasia.