Wakimbizi wa Syria wazuiliwa kuingia Uturuki

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu

Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmed Davutuglo, anasema kuwa zaidi ya watu 15,000 wamekusanyika kwenye mpaka wake, wakitoroka mashambulizi makali yanayoongozwa na Urusi, Kaskazini Mashariki mwa Syria.

Waziri huyo Mkuu anaamini kuwa makumi ya maelfu ya wakimbizi wengine wako njiani kuelekea kwenye mpaka huo.

Hadi kufikia sasa wakimbizi hao hawaruhusiwi kuingia Uturuki.

Image caption Wakimbizi wa Syria wanaokimbia vita katika mpaka wa Uturuki

Hata hivyo wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya Uturuki wameruhusiwa kuvuka mpaka na kutoa misaada kwa watu hao.

Wakimbizi hao walitimuliwa makwao wakati wanajeshi wa Syria,wakiungwa mkono na mashambulizi ya ndege za kijeshi za Urusi, walipotekeleza mashambulizi katika mji wa Allepo.