Mamake rais Assad wa Syria amefariki

Haki miliki ya picha .
Image caption Mamake rais wa Syria Assad afariki

Vyombo vya habari nchini Syria vinasema kwa mamake rais wa Syria Bashar al-Assad ameaga dunia mjini Damascus akiwa na umri wa miaka 86.

Anissa Makhlouf al-Assad alikuwa mjane wa rais wa zamani wa Syria Hafez Assad na wote walijaliwa jumla ya watoto sita.

Waandishi wa habari wanasema kuwa, amekuwa mgonjwa kwa miaka mingi na wakati mwingine alikuwa akisafiri kwenda nchini Ujerumani kupata matibabu, hadi mwaka 2012 wakati alijumuishwa kati ya watu kutoka nchini Syria waliowekewa vikwazo vya kusafiri na muungano wa ulaya.