Korea Kaskazini kujaribu kombora la 'nuklia'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vyanzo vya kijasusi vya Korea Kusini vinasema kuwa Korea Kaskazini inatayarisha jaribio jengine la kombora la nuklia.

Vyanzo vya kijasusi vya Korea Kusini vinasema kuwa Korea Kaskazini inatayarisha jaribio jengine la kombora la nuklia.

Habari zinawadia chini ya saa 24 tangu Korea Kaskazini irushe kombora la masafa marefu, kinyume na maazimio ya baraza la usalama la umoja wa Mataifa.

Shirika la habari la Korea Kusini, linaarifu kuwa idara ya ujasusi imetoa taarifa hizo mbele ya bunge.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shirika la habari la Korea Kusini, linaarifu kuwa idara ya ujasusi imetoa taarifa hizo mbele ya bunge.

Shirika hilo la kijasusi linasema kuwa Korea Kaskazini tayari imeshajipatia teknolojia ya kurusha kombora yenye uwezo kufika bara la pili.

Hatua hiyo ililaaniwa na mataifa kadha jirani na yale ya Magharibi.

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa linapanga kukutana baadaye leo kujadili matukio haya ya hivi punde.