Korea Kusini yaomba ulinzi wa makombora

Haki miliki ya picha EPA KCTV
Image caption Korea Kusini yaomba ulinzi wa makombora

Korea Kusini inasema kuwa itafanya mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kufanyika kwa ushirikiano na Marekani.

Mazoezi hayo yatakayodumu kwa zaidi ya kipindi cha miezi miwili yanalenga kujibu tishio kutoka Korea Kaskazini.

Mazoezi hayo yatafanyika kuanzia mwezi Machi hadi Aprili na kuwajumuisha wanajeshi maalum wa Marekani.

Pia maafisa wa Ulinzi wa Korea Kusini na Marekani wanasema kuwa wataanzisha mazungumzo kuhusu uwezekano wa kupelekwa kwa mitambo ya hali ya juu ya kukabiliana na makombora ili kujikinga dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha US Mil
Image caption Mfumo huo mpya wa ulinzi dhidi ya mashambulizi ya makombora almaarufu Terminal High Altitude Area Defence (THAAD) unatokea Marekani.

Mfumo huo mpya wa ulinzi dhidi ya mashambulizi ya makombora almaarufu Terminal High Altitude Area Defence (THAAD) unatokea Marekani.

Afisa wa ulinzi wa Korea Kusini Ryu Je-seung alisema kuwa mitambo hiyo ambayo itawekwa katika rasi ya Korea itatumiwa tu dhidi ya Korea Kaskazini.

Katika miaka ya awali China na Urusi z ilipinga vikali kuwekwa kwa mtambo huo wa kisasa zaidi karibu na mipaka yake.

Urusi na China zinaonya kuwa kuwepo kwa mitambo hiyo katika rasi hiyo huenda ikachangia mashindano ya silaha na hata labda vita.