Misikiti yawaalika wasio waislamu Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Zaidi ya misikiti 90 kote nchini Uingereza itafungua milango yake kwa wale wasio waislamu ilikujaribu kuondoa chuki dhidi ya uislamu.

Zaidi ya misikiti 90 kote nchini Uingereza itafungua milango yake kwa wale wasio waislamu ilikujaribu kuondoa chuki dhidi ya uislamu.

Shughuli hiyo inaandaliwa na baraza la waislamu la Uingereza ambalo linasema kuwa mashambulizi mengi yanayotekelezwa dhidi ya waislamu huwafanya watu kuwa na shaka kwa dini hii.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Karibu mwaka moja sasa visa vya kulengwa kwa waislamu vimeongezeka sana nchini humo.

Karibu mwaka moja sasa visa vya kulengwa kwa waislamu vimeongezeka sana nchini humo.

Misikiti itatoa fursa kwa watu kuelewa uislamu na pia watu wataruhusiwa kufuatilia maombi au kupata kikombe cha chai.

Idadi ya Misikiti inayoendesha mpango huo imeongezeka mara tatu kuliko mwaka uliopita.

Mpango huu mahsusi unafwatia kwa karibu maandamano ya amani yaliyofanywa na chama cha wazungu wanaopinga kuwepo kwa Waislamu barani ulaya Pegida, katika mji wa Birmingham Jumamosi.

Image caption Kuna takriban waisilamu milioni tatu nchini Uingereza.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa idadi ndogo ya watu ndio waliojitokeza katika maandamano hayo lakini Waislamu wameamua kufungua milango ya misikiti ilikuwaruhusu raia kuuliza maswali wanayotaka .

Kuna takriban waisilamu milioni tatu nchini Uingereza.

Waislamu hao ni aslimia 5% ya raia wa taifa hilo.

Takwimu zinaonesha kuwepo kwa misikiti 1,750 kote nchini humo.

Image caption Takwimu zinaonesha kuwepo kwa misikiti 1,750 kote nchini humo.

Misikiti iliyoko katika miji mikubwa ya London, Birmingham, Manchester, Leeds, Glasgow, Cardiff na Belfast zinashiriki siku hii ya uwazi.

Sheikh Sajjad Amin, kutoka msikiti wa Khizra ulioko Manchester alisema kuwa wanakusudia kutangamana na jamii karibu na misikiti yao.