Rubio taabani katika mdahalo wa Republican

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rubio taabani katika mdahalo wa Republican

Mdahalo wa wagombea wakuu wa chama cha Republican umeishia ubishi mkali baada ya wawaniaji kiti cha urais wa chama hicho kuelekeza mashambulizi kwa mgombea aliyemaliza katika nafasi ya tatu katika kura za mashinani katika jimbo la Iowa jumatatu iliyopita seneta Marco Rubio.

Gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie alisema kuwa kuimarika kwa seneta Rubio, ni hatari kwani hana ujuzi wowote .

Mwakilishi huyo wa jimbo la Florida hakusazwa na mpinzani wake mkuu Donald Trump na Jeb Bush.

Mdahalo huo ulifanyika siku nne tu kabla ya mchujo wa pili wa mgombea atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican katika uchaguzi mkuu ujao.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mgombea Donald Trump alionekana mtulivu kidogo

Asilimia kubwa ya wagombea saba wakuu katika chama cha Republican nchini Marekani walibadilishana zamu ya kumshambulia seneta huyo ambaye anadaiwa kukosa msimamo katika maswala makuu yanayohitajimaamuzi magumu.

Gavana wa Florida Marco Rubio ambaye alijiongezea umaarufu baada ya uteuzi wa jimbo la Iowa alionekana kukasirishwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa washindani wake.

Mgombea Donald Trump alionekana mtulivu kidogo baada ya kupoteza uteuzi katika jimbo la Iowa kwa seneta wa Texas Ted Cruz.

Wagombea walikabiliana katika masuala kadha yakiwemo afya, uhamiaji utoaji mimba na kuhusu ni nani aliye na tajriba ya kuongoza nchi.