Uturuki yatakiwa iwapokee wakimbizi wa Syria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uturuki yatakiwa iwapokee wakimbizi wa Syria

Rais wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa nchi yake iko tayari kuwapokea maelfu ya wakimbizi ambao wanakimbia mapigano makali katika maeneo ya Aleppo.

Uturuki inakataa kuwaruhusu hadi wakimbizi 35,000 kuvuka mpaka ikisema kuwa inawapa chakula na makao watu walio upande wa Syria.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Uturuki inakataa kuwaruhusu hadi wakimbizi 35,000

Maafisa nchini Uturuki wanasema kuwa wakimbizi hao wanapewa chakula na makao ndani ya ardhi ya Syria na hakuna haja ya kuwaruhusu wavuke mpaka.

Mwandishi wa Habari wa BBC aliyeko huko anasema kuwa Uturuki imefunga mpaka wake ilikujaribu kuangazia swala la wakimbizi wanaohangaika kufuatia mashambulizi makali ya majeshi ya serikali ya Syria yakisaidiwa na ndege za Urusi.

Image caption Uturuki inakataa kuwaruhusu hadi watu 35,000 kuvuka mpaka

Wanasiasa kutoka nchi za muungano wa ulaya wametoa wito kwa serikali ya Uturuki kuwaruhusu wakimbizi kutoka Syria kuingia nchini humo.

Mkuu wa sheria za muungano wa Ulaya, bi Federica Mogherini alisema kuwa kuna jukumu la kibinadamu kutoa ulinzi kwa wakimbizi.

Uturuki imejipata katika hali tata kwani inatazamiwa kuzuia wakimbizi kutoka Syria wasiende ulaya huku vile vile ikitarajiwa kutoa hifadhi kwa mamilioni ya watu wanaohangaishwa na vita

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa nchi yake iko tayari kuwapokea

Nchi hiyo tayari imewahifadhi zadidi ya wakimbizi milioni 2.

Wakimbizi wanazidi kuongezeka katika kambi mpya ambayo imeibuka katika mpaka wa Uturuki an Syria tangu maelfu ya watu waanze kuukimbia mji wa Allepo.

Wanaharakati wanasema kwa zaidi ya watu 400 wameuawa tangu mashambulizi ya serikali yanayoungwa mkono na Urusi yaanze Jumatatu iliyopita mjini Allepo.