India yazima huduma ya bure ya Facebook

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini India imeifunga huduma ya bure ya mtandao wa kijamii wa Facebook.

Mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini India imeifunga huduma ya bure ya mtandao wa kijamii wa Facebook.

Idara hiyo inasema kuwa kuwepo kwa mtandao wa bure unaogharamiwa na Facebook unakiuka uhuru wa mtandao intanet.

Huduma hiyo inayotolewa na Facebook inaruhusu watumiaji kutembelea anuani chache tu kwenye mtandao wa intaneti.

Wakosoaji wa huduma hiyo wanasema kuwa inawanyima wahindi uhuru wa kutembelea mitandao mingine.

Image caption Ankhi Das msemaji wa Facebook Kusini mwa Asia

Huduma hiyo ilikuwa inawaruhusu watumiaji kutembelea mitandao ya habari ambayo tayari imeshachaguliwa ,mitandao ya utabiri wa hali ya hewa ,Mtandao wa BBC, Wikipedia na mitandao inayotoa huduma za kiafya.

"Hakuna kampuni inayotoa huduma za intaneti itakayoruhusiwa kutoza ada ya aina yeyote watumiaji kwa ajili ya kupokea huduma hiyo'' uamuzi wa mamlaka inayosimamia huduma ya mawasiliano ya india (Telecom Regulatory Authority of India (TARI ).

TARI inaendelea na uchunguzi kutathmini iwapo habari kwenye mitandao inapaswa kupewa kipau mbele.

Vikas Pandey, mzalishaji wa habari za mtandao wa BBC nchini India anaarifu kuwa kumekuwa na kampeini kubwa ya kupinga na kuunga mkono huduma hiyo ya Facebook .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwazilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg amekuwa akisisitiza kuwa ''haiwezekani kupeana mtandao wote wa intanet bure''.

Kwa wakati mmoja Facebook ililazimika kununua matangazo ya kibiashara ilikutetea huduma hiyo yake.

"watu wanaoishi mijini ndio wanaoitumia sana mtandao wa intanet.

Lakini huwezi kuwapa mtandao wa intaneti watu wanaoishi vijijini kisha uwadhibiti wanaweza kutembelea mitandao gani na kususia mitandao mingine na kuwashurutisha kutembelea mitandao fulani na kuwanyima ruhusa ya kutembelea mitandao wanayotaka wenyewe,, sio haki wanaopinga mradi huo wanasema.

Mwazilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg amekuwa akisisitiza kuwa ''haiwezekani kupeana mtandao wote wa intanet bure''.

Facebook ilikuwa ikikusudia mpango huu wake wa Internet.org ulioanzishwa mwaka wa 2013 katika mataifa 36 kote duniani utawawezesha watu milioni 15 kutembelea mtandao wa intaneti.