Watu sita wajeruhiwa na chui India

Huwezi kusikiliza tena

Watu sita wanauguza majeraha nchini India baada kushambuliwa wakijaribu kumdhibiti chui aliyekuwa ameingia kwenye shule moja.

Mwanasayansi na mfanyakazi wa idara ya misitu ni miongoni mwa watu wanaouguza majeraha baada ya kukabiliana na chui huyo kwa karibu saa 10 Jumapili.

Haki miliki ya picha Kashif Masood
Image caption Maafisa wa wanyamapori wanasema huenda chui huyo alitoka msitu ulio karibu

Chui huyo, aliyeingia shule ya Vibgyor, baadaye alidungwa sindano ya kumtuliza na kisha akaachiliwa arejee porini.

Sensa ya wanyama mwitu iliyofanywa majuzi nchini India inakadiria idadi ya chui kuwa kati ya 12,000 na 14,000.

Chui huyo mwenye umri wa miaka minane alionekana akiingia kwenye shule hiyo katika eneo la Kundalahalli, kwenye kanda ya video.

Haki miliki ya picha Reproducao

Kanda hiyo ya video iliyonaswa na kamera za usalama kwenye shule hiyo ilimuonyesha chui huyo akimshambulia mwanamume karibu na kidimbwi cha kuogelea.

Afisa wa wanyama pori Ravi Ralph ameambia mwandishi wa BBC Hindi Imran Qureshi kwamba chui huyo huenda alitoka kwenye msitu ulio karibu.

Baada ya kukamatwa, alipelekwa kwenye mbuga ya taifa.

Haki miliki ya picha Kashif Masood

Chuo na wanyama wengine wamekuwa wakiingia maeneo ya makazi India.

Mwaka uliopita, chui mwingine aliyeingia kwenye kijiji kimoja jimbo la Rajasthan, kaskazini mashariki mwa India, alipatikana kichwa cha kikiwa kimekwama kwenye chungu katika kijiji kimoja.