Aliyenunua kobe aliyeibiwa Australia amrejesha

Kobe Haki miliki ya picha Perth Zoo
Image caption Kobe huyo aiibiwa Jumanne wiki iliyopita

Mtu aliyenunua kobe, bila kujua kwamba kobe wa aina hiyo wamo katika hatari ya kuangamia, amemrejesha kwenye hifadhi ya wanyama.

Kobe huyo alikuwa ameibiwa kutoka kwenye hifadhi ya Perth Zoo nchini Australia na kuuzwa kwenye soko la magendo.

Maafisa wamemtaja mwanamume huyo kuwa Msamaria Mwema kwa kuhakikisha kobe huyo amerejeshwa kwenye hifadhi hiyo.

Alipoteza pesa alizotumia kumnunua kobe huyo mwenye umri wa miaka kumi.

Wahudumu wa Perth Zoo wanaamini kobe huyo ambaye gamba lake lina rangi ambayo imesambaa kama nusuvipenyo aliibiwa Jumanne wiki iliyopita.

Hii si mara ya kwanza kobe kutoweka kutoka kwenye hifadhi hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Asili ya kobe hao ni Madagascar

Mwaka 2011, kobe wawili waliibiwa.

Asili ya kobe wa aina hiyo ni kisiwa cha Madagascar na wamo hatarini kutokana na kuharibiwa kwa maeneo ambayo wanaishi pamoja na ujangili.