Je Suu Kyi atakuwa rais wa Burma?

Image caption Bunge la Burma limetangaza kuwa halitamchagua rais mpya hadi katikati ya mwezi Machi.

Bunge la Burma limetangaza kuwa halitamchagua rais mpya hadi katikati ya mwezi Machi.

Taarifa rasmi haijatolewa kuhusiana na nini haswa kimesabibisha chama hicho kufikia uamuzi huo wa kuahirishwa kwa zoezi hilo.

Hatua hiyo itachochea zaidi matarijio kuwa cha bi Aung San Suu Kyi aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa, kitajaribu kuwasilisha mswada utakaondoa kwa muda vikwazo vinavyomnyima haki ya kuwa rais wa taifa hilo.

Licha ya kuongoza chama chake cha National League for Democracy kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Katiba ya sasa haimruhusu bi Suu Kyi kugombea kiti hicho kwa sababu watoto wake wawili wa kiume wana uraia wa Uingereza.

Katiba ya sasa haimruhusu bi Suu Kyi kugombea kiti hicho kwa sababu watoto wake wawili wa kiume wana uraia wa Uingereza.

Muhula wa rais wa sasa Thein Sein utakamilika mwishoni mwa mwezi Machi na mchakato wa kuwachagua viongozi wapya utaanzishwa na bunge tarehe kumi na saba mwezi Machi.