Mtanzania auawa kwenye kasino Nairobi

Kilimanjaro
Image caption Mtanzania huyo alitoka mkoa wa Kilimanjaro

Raia wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.

Alijaribu kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa rehani, walioshuhudia wanasema.

Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh.

Image caption Mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari

Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.

Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.

Polisi wamesema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kama John Barnabas mwenye umri wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Huwezi kusikiliza tena

Alikuwa akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.

Kabla ya kisa hicho, waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema alikuwa ameuza pikipiki hiyo ili kupata pesa za kwenda kucheza kamari.