Watu wanane wafariki ajali ya treni Ujerumani

Ajali Haki miliki ya picha EPA
Image caption Polisi wanasema watu wawili wamefariki

Watu wanane wamethibitishwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya treni mbili za kubeba abiria kugongana katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bad Aibling, takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.

Polisi wa Bavaria wameandika kwenye Twitter kwamba watu wanane wamefariki, watu zaidi ya 50 wakaumia vibaya na takriban watu 100 wana majeraha madogo.

Moja ya treni hizo ilitka kwenye reli baada ya ajali hiyo na mabehewa yake yakabingiria, vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wengi wa huduma za dharura wametumwa eneo hilo

Inaaminika magarimoshi hayo yaligongana ana kwa ana.

Maafisa wa kutoa huduma za dharura wamefika eneo la ajalii na helikopta zinatumiwa katika uokoaji.

Barabara zilizo karibu na eneo hilo zimefungwa, sawa na njia ya reli kati ya miji ya Holzkirchen na Rosenheim.