UN yaonya mataifa dhidi ya IS

Haki miliki ya picha US ARMY

Umoja wa mataifa na Jeshi la marekani limeonya kuhusu mfumo binafsi wa wanamgambo wa islamic state ni kupata wafuasi barani Afrika na kutafuta ushirikiano mkubwa kutoka kwenye vikundi vingine vya ugaidi.

Umoja wa mataifa unalaani hatua hiyo ya kujiimarisha kwa kundi hilo la IS na kusema kwamba inatokana na kutokuwa na utawala madhubuti nchini Libya.

Huku,Jeshi la Marekani likitaka ushirikiano wa kikanda ili kupambana na wanamgambo wa kiislamu wa IS na Boko Haram walioko nchini Nigeria.

Polisi nchini Nigeria wanaarifu kuwa wamemkamata mwanafunzi mmoja ambaye walimshuku kuwa ni mfuasi wa wanamgambo wa IS,Polisi walianza kumtilia wasiwasi mwanafunzi huyo pamoja na wanaume wengine watatu kutokana na safari yao kuelekea nchini libya kwenye kambi ya mafunzo.