Historia ya Bernie Sanders

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani bwana Bernie Sanders

Je unamfahamu Bernie Sanders?

Seneta wa jimbo la Vermont nchini Marekani bwana Bernie Sanders ni muaniaji kiti cha urais wa chama cha Democrats.

Bwana Sanders ndiye mpinzani mkuu wa bi Hillary Clinton ambaye alikuwa amepigia upatu na wengi kuwa mwakilishi wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao wa urais.

Sanders alichaguliwa kwa mara ya kwanza kama mwakilishi mwaka wa 1990.

Bernie Sanders alitangaza nia yake ya kuwania urais wa Marekani mwezi Mei mwaka uliopita.

Na tangu hapo hakutazamwa kama mwenye uwezo wa kutwaa ushindi wa chama hicho cha Democrats kufuatia kile kilichotazamwa kama urithi wa bi Hillary Clinton.

Kwa mtazamao wa wapiga kura wengi Sanders alipata umaarufu mkubwa mno haswa baada ya kunadi sera ya kuvunja ''utawala wa wanasiasa mabilionea ''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sanders akipokea matokeo ya New hampshire kwa furaha

Kulingana naye bi Clinton alikuwa mgombea tajiri asiyejali hali halisia ya maisha ya mamilioni ya wamarekani maskini.

Sera hizo ziliibuka katika mijadala aliyoshiriki kukabiliana na bi Clinton.

Sanders ni Mmarekani myahudi.

Alizaliwa mjini Brooklyn, New York.

Amekiri mara nyingi kuwa ile hali ya kuishi katika nyumba ndgo sawa na mamilioni ya wamarekani ndiyo iliyojenga mawazo akilini mwake ya kuwepo aina mbili ya wamarekani ;

Wamarekani wa kawaida na wam

Alihitimu katika chuo kikuu cha Chicago,na katika miaka ya 60 na 70 alishiriki katika kampeini kadhaa za kupigania haki za kimsingi za kibinadamu ikiwemo maamndamano makubwa ya kupinga vita yaliyofanyika mwaka wa 1963.

Wakati wa vita vya Vietnam aliomba ruhusa ajiunge na jeshi iliashiriki katika vita hivyo lakini ombi hilo likakataliwa akisemekana kuwa ni ''Mzee''.

Sanders alijiunga na siasa mwaka wa 1971.

Haki miliki ya picha AFPGetty
Image caption Bwana Sanders alimshinda mgombea mwenza bi Hillary Clinton katika mchujo wa New Hampshire

Wakati huo aliwania kiti cha mwakilishi wa jimbo la Vermont akitumia chama cha Liberty Union , Chama ambacho kilifahamika kwa kuwa chenye kuegemea sera za kisosholisti na kilichopinga kushirikishwa kwa wanajeshi wa Marekani katika vita.

Alishindwa.

Alijaribu mara kadha kuwa gavana wa jimbo hilo hilo akashindwa.

Alimuoa mke wake bi Jane O'Meara Driscoll,katika mwaka wa 1988 .

Alitajwa na wengi kuwa mshauri wake mkuu wa kisiasa.

Mkurugenzi huyo mkuu wa chuo cha Burlington na seneta Sanders walijaliwa kupata watoto wanne kutoka ndoa zao za awali.

Alifaulu kuchaguliwa rasmi kama mwakilishi mwaka wa 1990 kama mwakilishi huru wa kwanza katika jumba la wawakilishi katika kipindi cha miaka 40.

Aliongoza hadi mwaka wa 2007 alipotwaa kiti cha seneti.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Seneta wa Vermont Bernie Sanders, aliyemshinda Hillary Clinton, amesema ushindi wake unaonesha watu wanataka “mabadiliko kamili”.

Tangu awasili Washington, Sanders alikuwa mstari wa mbele kuwakosoa viongozi wa vyama vya Republican na Democratic kwa kupendelea matajiri ,kuunda sera za kulinda makampuni na mashirika yanayohusishwa na mabwenyenye wakati wakitupilia mbali matakwa ya mamilioni ya raia maskini waliowengi.

Mara nyingi amepuuzilia mbali kuwa mbishi na mtu asiyeheshimu viongozi walioko madarakani.

Tangu ajiunge na siasa amekuwa kiongozi anayejitegemea aliyehudumu katika bunge la Congress kwa kipindi kirefu zaidi.

Mwaka wa 2010, alisimama na kuhutubia bunge la Congress kwa zaidi ya saa 8 na nusu akijaribu kupinga kuongezwa kwa kodi ya malipo yaliyokuwa yamependekezwa na aliyekuwa rais wakati huo George Bush.

Klingana na sanders mabadiliko hayo ya sera za kodi na malipo ya ushuru yalikuwa yanawafaidisha zaidi matajiri na kuwaongezea mzigo maskini.

Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 74 ameahidi kumaliza pengo kati ya matajiri na maskini, kutoa elimu ya vyuo vikuu bila malipo na ‘kuvunja’ benki kubwa kubwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sanders ndiye mpinzani mkuu wa bi Hillary Clinton

Mwaka wa 2013 Sanders akiwa mwenyekiti wa kamati yabunge ya kuwakilisha wanajeshi wa zamani aliisadia bunge kuimarisha matibabu na msaada wa kifedha kwa wanajeshi walijeruhiwa vitani na wale wanaohitaji matibabu.

Alipinga vikali vita vya Iraq.

Anafahamika kwa kusifu sana sera za kisoshiolisti zinazowapa raia wa mataifa ya Ulaya (NORDIC) malipo wakijaaliwa kupata watoto mbali na kutoa huduma ya bure ya Afya kwa watu wote.

Amekosolewa na wengi kwa sababu ya kimya chake kuhusiana na matatizo yanayosababishwa na umiliki huru wa bunduki nchini Marekani.