Boko Haram waua 11 Cameroon

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Boko Haram waua 11 Cameroon

Watu kumi na mmoja wameuawa wakiwemo washambuliaji wawili wa kujitolea, katika shambulio la bomu lililotokea nchini Cameroon.

Shambulio hilo lilitokea mjini Nguechewe ulioko Kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mpaka na Nigeria..

Watu wengine wengi walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo ambalo linaaminika kutekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.

Zaidi ya watu 30 walijeruhiwa wakati wa mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga katika eneo ambalo mara kwa mara linakumbwa na uvamizi wa wanamgambo wa Boko Haram, duru za kiusalama zilidokeza.

Duru hizo za kiusalama pia zilisema wavamizi hao wa kujitolea mhanga, ambao walikuwa wanawake, pia waliuaua.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wavamizi hao wa kike walijilipua mwendo wa saa kumi na mbili na dakika ishirini hivi alfajiri

Wanavijiji walikuwa wakikesha usiku wakati wavamizi wawili wa kujitolea mhanga walipojiunga nao, wakijifanya wao ni baadhi ya jamii.

Wavamizi hao wa kike walijilipua mwendo wa saa kumi na mbili na dakika ishirini hivi alfajiri, wakati ambapo wanavijiji ambao walikuwa wamekesha usiku kucha wakiandaa mlo.

Duru za kiusalama katika eneo hilo zilisema watoto wengi, akiwemo mvulana wa miaka sita na mwingine miaka 15, ni miongoni mwa waliouaua.

Mmoja wa wanachama wa kamati ya kiuslama iliyoundwa kukabiliana na mashambulizi ya Boko Haram pia aliuaua.

Image caption Hili ni shambulio la tano la kujitolea mhanga katika eneo la mbali la kaskazini mwa Cameroon tangu mwaka huu uanze.

Wale waliopata majeraha mabaya walisafirishwa hadi kwenye hospital kuu ya eneo hilo mjini Maroua.

Hili ni shambulio la tano la kujitolea mhanga katika eneo la mbali la kaskazini mwa Cameroon tangu mwaka huu uanze.

Mnamo Januari 18, watu wanne waliuaua wakati wa uvamizi kwenye msikiti wa Nguetchewe.

Takribani watu 1200 wameuaua tangu wanamgambo wa kiislamu wa kundi la Boko Haram kuanza kutekeleza mashambulizi katika taifa jirani la Cameroon, hii ni kwa mujibu wa takwimu za serikali.